Kamati ya Bunge kuhusu maswala
ya bajeti ya serikali, imekataa pendekezo la kuidhinisha pesa za
kumnunulia rais Mstaafu Mwai Kibaki, ofisi ambayo itagharimu shilingi
milioni miasaba za Kenya au dola milioni nane
Rais mstaafu alitengewa pesa hizo katika bajeti ya ziada iliyowasilishwa bungeni Jumanne wiki jana.Walichojaribu kufanya katika bajeti hii ni kutumia pesa za maendeleo kwa miradi mingine ikiwemo ujenzi wa opfisi ya rais mstaafu.
Kamati hiyo pia iligundua kuwa moja ya mambo yaliyofanya na hazina ya serikali ni kutenga dola milioni nane kwa baraza na mawaziri kwa ununuzi wa jengo
Katibu wa baraza la mawaziri Francis Kimemia alitetea bajeti hiyo akisema kuwa ofisi inapaswa kununuliwa kwa ajili ya mikutano ya mawaziri.
Pia Kimemia alisema kuwa chini ya sheria, rais mstaafu anapaswa kuwa na ofisi, awe na katibu wake na wafanyakazi watakao simamia mipango yake kama alivyofanyiwa rais mstaafu Daniel Moi.
Kimemia aliambia shirika la habari na Nation nchini Kenya kuwa dola milioni nane ni pesa kidogo sana kwa ununuzi wa jengo lolote na kuwa alidhani kamati ingemwambia hizo ni pesa kidogo sana. Kimemia alisema hawana budi ila kumnunulia rais mstaafu ofisi kwa sababu hakuna jengo walilonalo kwa sasa kumkabidhi Kibaki.
Kimemia alisisitiza kuwa serikali imekuwa ikimtafutia ofisi yenye bei nafuu rais Kibaki mjini Niarobi kwani ofisi zote zilizopo sasa zinagharimu shilingi bilioni 1
No comments:
Post a Comment