Kikosi kilichotarajiwa
kuwakilisha Kenya kwenye michuano ya kilabu bingwa Afrika, Tusker F.C
wamesema rasmi kuwa wamejiondoa kwenye michuano hiyo inayotarajiwa
kuchezwa nchini Sudan mwezi ujao.
Kwenye taarifa iliyotolewa na mkuu wa kilabu
hiyo, Charles Obiny , kilabu hiyo imejiondoa kwa sababu ya kiusalama
zinazotokana na mgogoro katika jimbo la Dafur, ambako walitarajiwa
kuchezea mechi zao.Wanasema eneo hilo sio salama.
Hatua ya kilabu ya Tusker, inakuja licha ya hakikisho kutoka kwa Bwana Magdi Shams Eldin katibu mkuu wa wa ligi ya soka ya Sudan katika barua iliyoandikwa kwa vilabu vyote tarehe 23 Mei mwaka huu.
Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda la Kenya, Sam Nyamweya amethibitisha kuwa, amepokea ombi kutoka kwa kilabu ya Tusker ikielezea wasiwasi wa usalama wakisema kuwa hawawezi kuruhusu wachezaji wao kucheza katika eneo lenye utovu wa usalama na ni juu ya CECAFA kutafuta sehemu nyingine iliyo salama kwa wachezaji kutoka vibau vyote kuweza kushiriki michuano hiyo
No comments:
Post a Comment