Monday, June 17, 2013

AKUTWA AMEKUFA NYUMBA INAYOJENGWA, KIGOGO, DAR



Kijana mmoja aliyefahamika wa kwa jina la Kobero, leo asubuhi amekutwa akiwa amekufa kwenye chumba kimoja cha nyumba ambayo ilikuwa haijamalizika kujengwa maeneo ya Kigogo Luhanga jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, marehemu alikutwa na chupa iliyokuwa na masalia ya pombe haramu aina ya gongo. Mpaka paparazi wetu anaondoka eneo la tukio askari polisi walikuwa bado hawajafika kwa ajili ya kuuchukua mwili na kuanza upelelezi wa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment