Na Khatimu Naheka
KIUNGO mshambuliaji wa Ivory Coast, Salomon Kalou, ameshukuru ushindi wa mabao 4-2 ilioupata timu yake dhidi ya Taifa Stars, lakini akashtushwa na uwezo wa nyota wa timu hiyo, beki Shomari Kapombe wa Simba.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Stars mwishoni mwa wiki iliyopita kukubali kichapo hicho katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia mwakani ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kalou anayekipiga katika kikosi cha Lille nchini Ufaransa, ameshtushwa na uwezo wa Kapombe ambapo kwa muda wa dakika tisini aligundua kuwa nyota huyo ana siri kubwa mbili ambazo zimemshtua.
Kalou…

Kalou alisema katika mchezo huo, Kapombe alionyesha uwezo mkubwa katika kipengele cha ukabaji, lakini akashangaa pia nyota huyo akionyesha uwezo mkubwa katika kupandisha mashambulizi ambapo moja ya krosi zake tatu alizopiga katika mchezo huo, ilizaa bao, lililofungwa na mshambuliaji Thomas Ulimwengu.
“Nimekutana na mabeki wengi wadogo wazuri lakini yule mwenye namba ishirini (Kapombe) ana sifa kama mabeki wengi tunaocheza nao Ulaya, ana akili sana katika ukabaji, nilimfuata mara mbili lakini hakunipa nafasi ya kumpita kirahisi, amejitahidi sana leo (Jumapili),” alisema Kalou na kuongeza:
“Ukiacha hilo, pia alinishangaza, kumbe alikuwa ni mkali sana katika kupandisha mashambulizi.
“Nilishangaa ile krosi aliyopiga ikazaa bao, niliona kama mabeki wetu watamzuia, lakini ilishindikana, nimefurahishwa na uwezo walioonyesha Tanzania lakini nashukuru tumefikisha malengo yetu kwa kupata pointi tatu.”

No comments:
Post a Comment