Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Wilfred Muganyizi Lwakatare, jana alipokelewa kwa shangwe na
wafuasi wa chama hicho katika Uwanja wa Ndege mjini Bukoba. Baadaye
Lwakatare alifanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara mkoani hapo katika
Uwanja wa Uhuru baada ya kutoka rumande kwa dhamana kutokana na kesi
inayomkabili ya kutaka kumwekea sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi,
Dennis Msaki. Maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba walihudhuria mkutano huo
ambapo Lwakatare alieleza mambo mengi ambayo amejifunza akiwa rumande.
No comments:
Post a Comment