Washukiwa wa kundi la wapiganaji
wa kiisilamu nchini Nigeria, wamewaua wanafunzi tisa , katika
shambulizi la pili ambalo limewalenga wanafunzi katika siku za hivi
karibuni.
Washambuliaji wanaoaminika kuwa wanachama wa
kundi la wapiganaji wa Boko Haram, waliwashambulia kwa risasi wanafunzi
hao waliokuwa wamevalia sare za shule katika shule moja viungani mwa mji
wa Maiduguri.Baadhi ya manusura walisema kuwa ilikuwa hatua dhidi ya kuibuka kwa makundi ya vijana wanaotoa ulinzi kwa raia mjini humo.
Eneo la Kaskazini mwa Nigeria, liko chini ya sheria ya hali ya hatari huku serikali ikijaribu kupambana na kundi la Boko Haram pamoja na harakati za makundi ya kiisilamu.
Mmoja wa walioshuhudia Ibrahim Mohammed alisema alikuwa darasani akifanya mtihani wakati watu hao walipovamia jengo hilo.
"niliona wanafunzi watano, waliokuwa wanafanya mtihani wakiuawa papo hapo.''
''Wanafunzi wengine, waliuawa walipokuwa wanaingia shuleni''
Wafanyakazi wa hospitalini walithibitisha kuona miili ya watoto tisa wakiwa bado wamevalia sare zao wakipelekwa katikia chumba cha kuhifadhia maiti Maiduguri.
Msemaji wa Boko Haram, aliwaambia waandishi wa habari kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi na onyo kwa vijana kwa kusaidiana na jeshi.
Makundi ya vijana wanaotoa ulinzi wamekuwa wakiwakamata washukiwa wa Boko Haram na kuwakabidhi kwa jeshi.
Msemaji wa jeshi alisema kuwa wale waliokabidhiwa kwa polisi watafikishwa mahakamani na kutendewa haki.
No comments:
Post a Comment