Wednesday, June 19, 2013

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WABUNGE 4 WA CHADEMA KWA KUSABABISHA VURUGU ARUSHA

Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia viongozi wanne wa CHADEMA na watu wengine huku likiendelea kuwatafuta wabunge wawili na watu wengine.

Jeshi la Polisi limesema limewatua nguvuni watu hao kwa makosa ya kuhutubia mkutano haramu wakati wa kuwaaga marehemu waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika eneo la Soweto jijini humo mwishoni mwa wiki.

Makosa mengine ni wanayotuhumiwa kwayo ni kufunga barabara na kuwashambulia askari polisi.

Amesema wataendelea kubaki korokoroni hadi uchunguzi utakapokamilika.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amewataja Wabunge wanaoshikiliwa ni pamoja na Tundu Lissu na Mustapha Akunai.

Wanaotafutwa ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambao waliponyoka mikono ya polisi.

No comments:

Post a Comment