Kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya ezi hizi,nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chafu ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori,lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.
Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa.
No comments:
Post a Comment