Tuesday, June 18, 2013

Uchumi wa Kenya kukuwa kwa 6%

 
Benki ya dunia imetoa utabiri huu ili kusaidia Kenya kujiendeleza kiuchumi
Kiwango cha Ukuwaji wa uchumi wa Kenya kinakisiwa kitakuwa kwa asilimia 6 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, kinyume na utabiri wa mapema kuwa nchi hiyo yenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki itakuwa kwa asilimia nne.
Kulingana na benki ya dunia, habari hii nzuri, imehusishwa pakubwa na uchumi thabiti wa Kenya pamoja na uchaguzi wa Kenya uliofanywa kwa amani mwezi Machi mwaka huu.
Afisaa mkuu mtendaji wa benki ya Dunia nchini Kenya Diarietou Gaye, ameitaka serikali ya Kentya kubuni mazingira yatakayoiwezesha nchi hiyo kuvutia uwekezaji, maendeleo , ongezeko la uzalishaji wa kawi kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiashara pamoja na kuwa na sera nzuri za kifedha na matumizi ya pesa.
Utabiri huu unakuja wiki moja baada ya Kenya kutengaza bajeti yake ambayo itahitaji mabilioni ya dola kuweza kutimiza mahitaji yake ikilinganishwa ma ukuwaji wake.
Hata hivyo, Benki hiyo imeonya dhidi ya viwango vya juu vya riba ambavyo vinadumaza ukuwaji kwani watu wanahofia kuchukua mikopo.
Makadirio ya sasa, yanakuja wakati Kenya inakabiliana na wakati mgumu kubuni nafasi za kazi kwa vijana pamoja na kuwa na mipango ya kupunguza viwango vya umaskini.
Miongoni mwa hatua zizlichukuliwa na serikali ni kubuni hazina ya pesa za maendeleo ya vijana na wanawake walio na azma ya kufanya biashara.
Ili wakenya waweze kufikia uchumi wa mataifa 20 yanayokuwa kwa kasi duniani ifikapo mwaka 2013, Benki ya dunia inasema kuwa sharti ipunguze viwango vya umaskini kwa asilimia mbili kila mwaka.
Hii ni ripoti ya nane ya benki ya dunia kutolewa kabla ya mwisho a mwaka inayonuia kusaidia Kenya kutimiza malengo yake ya ugatuzi.

No comments:

Post a Comment