Friday, June 7, 2013

NGUMI KUPIGWA SIKU YA TAMASHA LA MATUMAINI


Bondia Thomas Mashali (kulia) akitia saini ya dole gumba kwenye mkataba wa kupambana kwa ajili ya kuchangia elimu siku ya Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Julai 7, mwaka huu katika uwanja mpya wa Taifa jijini Dar. Mashali atacheza na Bondia Patrick Amote kutoka Kenya. Tamasha hilo litawashilikisha wasanii mbalimbali pamoja na wabunge. Kushoto ni Rais wa TPBO, Yasin Abdallah.
Bondia Francis Miyeyusho (kulia) akisaini mkataba kwa ajili ya mpambano wake na Bondia Shadrack Muchanje  kutoka Kenya katika Tamasha la Usiku wa Matumaini. Kushoto ni Rais wa TPBO, Yasin Abdallah.
Thomas Mashali akipokea sehemu ya fedha za maandalizi kwa ajili ya mpambano wake na Bondia Patrick Amote katika Tamasha la Usiku wa Matumaini.
Bondia Francis Miyeyusho (kulia) akipokea sehemu ya fedha za maandalizi kwa ajili ya mpambano wake na Bondia Shadrack Muchanje  kutoka Kenya.

No comments:

Post a Comment