Friday, June 21, 2013

MABOMU ARUSHA; LEMA NUSURA ATUMBUKIE KWENYE MAFUTA YA KITIMOTO

KUFUATIA mapambano ya raia na Jeshi la Polisi mjini hapa, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), Jumanne wiki hii alilazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe karibu na eneo hilo ambapo alidaiwa kunusurika kutumbukia kwenye mafuta ya kiti moto.
Lema aliyenusurika kupigwa na bomu lililoharibu gari lake, alikuwa akijaribu kuwatuliza wananchi walioanza kukusanyika katika vikundi, wakijadili amri ya serikali ya kukataza miili ya watu waliofariki dunia katika shambulio la bomu, isiagwe kwenye Viwanja vya Soweto, mjini hapa.

Kabla ya kupigwa mabomu na kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe hao, Lema alikuwa akiwataka wananchi kuwa wavumilivu…

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
KUFUATIA mapambano ya raia na Jeshi la Polisi mjini hapa, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), Jumanne wiki hii alilazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe karibu na eneo hilo ambapo alidaiwa kunusurika kutumbukia kwenye mafuta ya kiti moto.

Lema aliyenusurika kupigwa na bomu lililoharibu gari lake, alikuwa akijaribu kuwatuliza wananchi walioanza kukusanyika katika vikundi, wakijadili amri ya serikali ya kukataza miili ya watu waliofariki dunia katika shambulio la bomu, isiagwe kwenye Viwanja vya Soweto, mjini hapa.
Kabla ya kupigwa mabomu na kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe hao, Lema alikuwa akiwataka wananchi kuwa wavumilivu kwani walikuwa wanawasiliana na serikali ya mkoa ili kupata kibali cha kuaga miili ya wapendwa wao.
Ghafla polisi walifika na kutangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo ili kuweka hali ya usalama ambapo walisema pasingekuwa na suala la kuaga miili ya watu hao katika eneo hilo. Zoezi hilo lilikwama baada ya mabomu kurindima kwa mara nyingine.

No comments:

Post a Comment