Huyu mama alikaa juu ya paa kwa siku tatu tangu jumamosi kupinga nyumba
yao kuchukuliwa na bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu alipochukua mkopo
bank miaka mingi iliyopita na kushindwa kulipa mkopo huo.
Kwa mujibu wa maelezo yake kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa
alikopa ml 240 wameuza nyumba zake 2 na mabasi mawili.Wenyewe
wanachodai katika hilo deni imebaki tsh ngapi na wao watoe?kama nyumba
iuzwe watoe deni la bank na hela inayobaki wabaki nayo wao.
Nyumba ipo mbezi Tangi bovu na inaeneo kubwa sana mama anasema hata
akiuza si chini ya ml 500 iweje atolewe kwa ml 240?wakati mdaiwa nyumba
zake mbili zimeshachukuliwa na mabasi mawili yale makubwa ya safari za
mikoani.Hiyo ml 240 haijatimia tu?na kama bado kiasi gani kimebaki?
Ndani ya nyumba vitu walishachukua hao watu wa auction mart ndani
kweupe.Na wakati haya yakiendelea hakukuwa na amri yoyote iliyotoka
mahakamani wala hawakuwa na kibali cha mahakama.
Gea alimfata huko huko juu kumsikiliza na tumemsikia leo kwenye heka heka.Kesho pia itaendelea...
Chumba cha habari cha clouds fm kimeenda kufatilia hapo bank ya Tanzania Investment bank(TIB)kujua kulikoni??
Maana
wakati haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba
imeshauzwa.Inauzwaje na shauri lipo mahakamani?Na jana mume wa huyu mama
alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku ya kesi kuendelea kusikilizwa.
Na mumewe alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao virudishwe.
No comments:
Post a Comment