Friday, June 21, 2013
HAUSIGELI ATAKA KUJIRUSHA GHOROFANI
HAUSIGELI ambaye jina lake halikupatikana mara moja, nusura ajirushe chini kutoka ghorofa ya pili kwa kile kilichodaiwa kuwa aliogopa moto mkubwa uliozuka katika jengo la jirani na ghorofa alilokuwemo.
Tukio hilo lilijiri mapema asubuhi ya Juni 18, mwaka huu kwenye makutano ya Mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa majirani, baada ya kuona moto huo ulioambatana na wingu zito la moshi ukitoka kwenye jengo la jirani, hausigeli huyo alitoka dirishani na kutaka kujirusha chini bila kujali nguo zilizokuwa zikimvuka katika purukushani hiyo.
Alifanikiwa kukaa kwenye sehemu ya ukingo wa ghorofa hilo na kujiandaa kwa tukio la kwenda chini akiamini atakuwa amejiokoa na moto huo.
Hata hivyo, bosi wa hausigeli huyo alipoona zoezi hilo la hatari alitoa mkono dirishani na kumvutia ndani mfanyakazi wake huyo tukio ambalo lilijiri muda mfupi kabla ya Kikosi cha Zima Moto kufika na kufanikiwa kuuzima bila kujeruhi mtu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment