Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare amesema atatoa ya moyoni siku ya Alhamisi.
Akizungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi mara baada ya
kupata dhamana aliomba subira kwa watanzania kwani anayo siri nzito
moyoni.
Lwakatare alisema anawaomba waandishi wa habari watulie kwani
anatarajiwa kuzungumza kwanza na viongozi wake wakuu wa chama na jopo la
wanasheria wake nguli ndipo azungumze na dunia.
Wakati hayo yakiendelea mtandao wa You Tube unamuonyesha Naibu Katibu
Mkuu CCM Mwigulu Nchemba akitamba kwenye kampeni za udiwani Arusha
kwamba ndiye aliyegharamia vifaa vyote vilivyotumika kumrekodi Lwakatare
na hatimaye mateso yote yaliyomfika Lwakatare.
Viongozi wakuu wa Chadema tayari wameelezea furaha yao baada ya
Lwakatare kupata dhamana.Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe yuko
Dodoma katika vikao vya bunge wakati Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa yuko
kwenye ziara ya kichama barani Ulaya.Katika salamu zake jana alizozitoa
akiwa Ujerumani Dr Slaa alimpa pole Lwakatare na hapo hapo kuelezea
furaha yake na ya watanzania wanaoishi Ujerumani kwa Lwakatare kupata
dhamana na kuweza kuungana na familia yake tena baada ya mateso ya miezi
mitatu.
No comments:
Post a Comment