Wednesday, June 19, 2013

Juma Kaseja: Sina timu kwa sasa jamani

Kipa wa Simba, Juma Kaseja.
Na Khatimu Naheka

KIPA wa Simba, Juma Kaseja, amesema kwa sasa hawezi kujiunga mapema katika mazoezi ya kikosi hicho kutokana na kwamba hana mkataba na klabu yoyote.

Kauli hiyo ya Kaseja inakuja kufuatia kipa huyo mkongwe kumaliza mkataba wake wa kuitumikia Simba, ambao ulifikia tamati mwishoni mwa msimu uliopita.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kaseja alisema kwa sasa hawezi kujiunga mapema na kikosi hicho alichokitumikia hadi msimu uliopita kwa kuwa hana mkataba na timu hiyo baada ya ule wa awali kumalizika.

Kaseja alisema kwa sasa atakuwa na mapumziko ya siku chache baada ya kumaliza majukumu ya Taifa Stars, ambapo atajua hatima ya timu…
Kipa wa Simba, Juma Kaseja.
Na Khatimu Naheka
KIPA wa Simba, Juma Kaseja, amesema kwa sasa hawezi kujiunga mapema katika mazoezi ya kikosi hicho kutokana na kwamba hana mkataba na klabu yoyote.
Kauli hiyo ya Kaseja inakuja kufuatia kipa huyo mkongwe kumaliza mkataba wake wa kuitumikia Simba, ambao ulifikia tamati mwishoni mwa msimu uliopita.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kaseja alisema kwa sasa hawezi kujiunga mapema na kikosi hicho alichokitumikia hadi msimu uliopita kwa kuwa hana mkataba na timu hiyo baada ya ule wa awali kumalizika.
Kaseja alisema kwa sasa atakuwa na mapumziko ya siku chache baada ya kumaliza majukumu ya Taifa Stars, ambapo atajua hatima ya timu atakayoichezea msimu ujao ndani ya siku saba kuanzia juzi.
“Ukiniuliza nitajiunga lini katika mazoezi ya Simba, sidhani kama nitakupa jibu zaidi ya sijui, kutokana na sasa sina mkataba wowote na Simba, mimi sasa ni mchezaji huru, mkataba wangu na Simba ulishakwisha,” alisema Kaseja huku akiongeza kwa kusema:
“Hivi ninavyoongea na wewe (juzi jioni), ndiyo kwanza hata nyumbani kwangu sijafika, natoka katika kambi ya timu ya taifa, nataka kwanza nikapumzike kwa siku kadhaa na baada ya hapo nadhani ndani ya siku saba nitajua nini nifanye na wapi nitasaini.”

No comments:

Post a Comment