Hali ya ati ati imekumba timu ya
taifa ya soka ya Ethiopia huku kukiwa na wasiwasi ikiwa itaweza
kuendelea na safari ya kuwania nafasi ya kufuzu kushiriki kombe la dunia
nchini Barzil mwaka ujao au la. Hii ni baada ya shirikisho la soka
duniani FIFA kuwachukulia hatua za kinidhani wachezaji wa kikosi hicho
Jumapili.
Mapema hapo jana , Ethiopia waliicharaza Afrika
Kusini mabao mawili kwa moja mjini Addis Ababa na kujipatia nafasi nzuri
katika kinyang'anyiro cha kufuzu kwa kombe la dunia.FIFA pia inachunguza kikosi cha Togo na kile cha Equatorial Guinea kwa kosa sawa na hilo.
Ikiwa timu hizo zitapatikana na hatia huenda zikaathiriwa vibaya katika kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao Brazil.
Kesi dhidi ya Ethiopia inatia wasiwasi kwani ikiwa watapatikana na hatia huenda ndoto yao ya kushiriki kombe la dunia mwaka ujao ikaambulia patupu huku Afrika Kusini waliokuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010, wakashiriki kwa mara nyingine.
Kwa sasa Ethiopia wako na pointi tano mbele ya Afrika Kusini katika kundi A na Afrika Kusini itakuwa tu na ponti mbili nyuma ikiwa Ethiopia watakubali Bostwana kutwaa ushindi kwa kosa lao la kumchezesha mchezaji asiyefaa au asiyestahili kucheza.
Tangazo hilo la FIFA, halitaipa tu uhai timu ya Afrika Kusini bali wachezaji wa Cameroon na Cape Verde.Cameroon walicharazwa mabao mawili kwa nunge na Togo lakini timu hiyo huenda nayo ikapata pointi tatu zengine ikiwa Togio watapatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment