Saturday, May 4, 2013

WEMA AJINUNULIA MASHINE YA ‘MASAJI


Na Imelda Mtema
BEAUTIFUL Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu amejinunulia mtambo wa kufanyia masaji kwa lengo la kuondoa uchovu anaporejea nyumbani kwake akiwa amechoka.
Chanzo chetu makini kililitonya gazeti hili kuwa, kifaa alichonunua staa huyo ni mfano wa kiti ambacho mtumiaji anakaa na kukiseti anavyota kisha kinamuondoshea uchovu alionao.

“Yaani pale kwa Wema ukienda na uchovu wako unapelekwa kwenye kile kiti, wewe kazi yako unakaa tu na rimoti, unachagua ni wapi kikuweke sawa,” kilisema chanzo hicho.

Wema alipopigiwa simu na paparazi wetu kisha kuulizwa kuhusu kifaa hicho alikiri kukinunua na kueleza kuwa, amefanya hivyo ili kuokoa muda ambao angeutumia kwenda kufanyiwa kwenye vituo vya masaji vilivyopo mjini.

No comments:

Post a Comment