Thursday, May 16, 2013

Amri Kumi Kwa Wapendao Ofa ya Bia


    1. Muheshimu anayekununulia
    2. Muamkie mtoa ofa kabla hujakaa kitini
    3. Uwe ndie mchekeshaji wa kikao, lakini usimkatishe mazungumzo anaetoa ofaa
    4. Daima jitolee kufuata na kubeba vinywaji toka kaunta
    5. Mtoa ofa akikutuma popote usikatae
    6. Mtoa ofa akiupenda muziki fulani, we anza kucheza kwa bidii kabisa
    7. Usiwe msafi kuliko mtoa ofa
    8. Usinywe kwa pupa, kunywa mafunda madogomadogo
    9. Usitamani mpenzi wa mtoa ofa hata kama ndie mke wako
    10. Mtoa ofa akitoa kichekesho cheka sana hata kama hakichekeshi
    KUMBUKA……Mtoa ofa akiwa Man U na wewe Man U, akiwa Chelsea na wewe hivyo hivyo. Akiwa CCM na wewe onyesha kadi kabisa, akiwa CHADEMA onyesha kadi na katiba…kifupi uwe umejitayarisha kila wakati.

No comments:

Post a Comment