Matapeli wa kwenye mtandao wamuandama Wolper! Soma hapa kilichomtokea leo na alichosema kuhusu Facebook.
Katika
kile kinachoonekana ni mwendelezo wa matapeli wa mjini kutumia majina
ya waigizaji maarufu nchini kutapeli watu kwa njia ya mtandao, dhahama
hii sasa imemkuta mwanadada Jacqueline wolper baada ya watu wanaoaminika
kuwa ni matapeli kutumia jina lake kujipatia fedha na vitu vingine
kiudanganyifu.
Akizungumza kwa simu na tovuti ya bongomovies.com
mwanadada Jacqueline wolper alisema matapeli hawa sasa wameamua kutumia
mtandao wa instagram na mtandao mwingine wa kijamii uitwao badoo kwa
jina la “wolper gambe25” katika kutapeli watu kwa kuwaomba hela au
michango mbalimbali kupitia account hizo feki
“Leo nilikuwa
naenda saluni, baada ya kufika tuu, yule dada wa saluni akaanza
kunilalamikia kuwa mbona sijaenda kuchukua viatu nilivyomuagiza pamoja
na hela? Nikawa sijui cha kumwambia maana sikumuagiza viatu na wala
sijampigia simu kumwambia anitumie hela, ndipo aliponionesha huo ujumbe
kwenye simu yake na ndio nikagundua hizo account feki za hao watu
wanaoutumia jina langu kutapeli watu” Alisema Jack.
“Mimi sipo
facebook na wala sitarajii kujiunga, nawaomba sana mashabiki wangu wajue
hilo. Natumia mtandao wa instagram kwa jina la wolpergambe au
jacklinewolperjacklinewolper.” Alisisitza Wolper
Pia alisema kuwa
amendundua leo kuna mtu mwingine anayetumia jina lake kuomba watu
wamchangie kuhusu kampeni inayoitwa “Zinduka” na amewataka sana
mashabiki wake wasije wakafanya hivyo kwani mtu huyo ni mwizi na
analengo la kumchafulia jina lake.
No comments:
Post a Comment