Hayo ameyasema wakati akikabidhi kadi za uanachama kwa Tawi jipya la Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCOBS) mkoani Kilimanjaro.
Silaa amesema kumekuwa na tabia ya viongozi wa CCM kuonea aibu hata makosa yanapotendeka kwa viongozi wa ngazi za chama kwa kuogopa kufukuzwa uanachama.
Pia amesema kukosoana ni sehemu ya kuleta maendeleo katika jamii yoyote ambayo inajali demokrasia ya kweli
Mjumbe huyo wa NEC taifa amesema vyama vya upinzani nchini vimepata nguvu kubwa kutokana na baadhi ya watendaji wa CCM ngazi za vijiji, kata, wilaya na mikoa kushindwa kuwawajibisha viongozi wanapokosea kwa kuogopa kufukuzwa ama kutendea kitu chochote kibaya
Aidha Silaa alisema kitendo hicho kimewapunguzia heshima mbele ya wananchi walioamini kuwa wanzilishi wa demokrasia nchini kupitia kupiga kura hata kusababisha majimbo mengine kuchukuliwa na wapinzani.
Hata hivyo, Jerry Silaa katika kutoa kwake rai hiyo amewataka viongozi hao kukosoana kwa utaratibu na kwamba anayekosea aangaliwe kama yeye na sio kama chama kwani sio wote ni wachafu.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Steven Kazidi amesema kutokana na kutokosoana baadhi ya wanasiasa wametumia mwanya huo huo kuanzisha migomo katika vyuo vikuu hapa nchini kwa kudai kuwa CCM iliyoko madarakani ndio imeyaleta hayo.
Kazidi ameongeza kusema wanansiasa hao wameendelea kumwaga sumu yao kwa wanavyuo hao kuwa wataendelea kupata taabu endapo wataendelea kuichagua CCM
Pia Katibu huyo maarufu kwa jina la “OFFSIDE” amewataka wanavyuo hao kuzingatia elimu hadi watakapomaliza masomo yao na hatimaye wachague chama cha siasa ambacho kitawaletea maendeleo
Kazidi amehitimisha kwa kusema migomo na maandamano yanayofanywa na wavyuo kutokana na uchochezi wa kisiasa yamesababisha kuharibu miundombinu ya vyuo husika zikiwemo samani na majengo
Awali akisoma taarifa ya Wanavyuo wa MUCCOBS kwa niaba ya wanachama wa CCM mbele ya Mgeni Rasmi Jerry Silaa, David Waryoba amesema umefika wakati kwa Chama cha Mapinduzi kufanya maamuzi dhidi ya wanaokichafua chama kwa kutumia maslahi ya chama kufanya hujuma kwa wananchi kwa manufaa yao kwa kupora rasilimali za taifa.
Hatimaye Mgeni rasmi alihitimisha kwa kuwakabidhi kadi wanachama wapya 155 kutoka MUCCOBS.
Habari kwa hisani ya Wavuti.
No comments:
Post a Comment