Monday, May 20, 2013

MRISHO NGASA ATAMBULISHWA RASMI YANGA

Mrisho Ngasa akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi. (Picha na Yanga)
Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngasa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako…
Mrisho Ngasa akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi. (Picha na Yanga)
Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngasa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa miaka 3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.

Naye mwenyekiti wa mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb  amesema anashukuru kwa Ngasa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa mchezaji anayejitolea kwa moyo wake wote katika timu zake zote alizokuwa akichezea hali iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango cha hali ya juu.
Kwa kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea katika timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia kwa kusema kuwa Ngasa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.
Aidha Ngasa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na kunishangilia pia.

Nimeamua kurudi katika timu yanga ya zamani sababu ndio sehemu pekee wanaponisikiliza na kunithamini, timu niliyotoka pamoja na kucheza kwa moyo wangu wote bado viongozi wake hawakua na imani na mimi hicho ndo kilichonipelekea kurudi katika timu yangu ya Yanga.
Ngsa anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia Yanga katika msimu ujao.

No comments:

Post a Comment