Reginald Mengi '1m price for a nice tweet"
Upo kwenye Twitter? Kama haupo fanya haraka
ujiunge sababu kuna ulaji huko!! Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya
IPP, Reginald Mengi amesema kuanzia mwezi huu, atakuwa akitoa shilingi milioni 1 kwa kila tweet itakayomfurashia.
Not to fast
though…… Sio tweet zile za ‘I’m having fun being single, #TeamSingle, tupa
kuleee!
Mengi anataka ulikune
jicho lake kwa tweet yenye akili ambayo inaweza kuchangia kwa namna moja ama
nyingine kupunguza umaskini uliokithiri nchini.
“Umaskini umekuwa sugu. Kwa mwaka 1 anzia Mei ntatoa sh 1m
kila mwezi kwa tweet nitakayochagua kuwa bora kushinda vita na umaskini,”
ametweet leo.
Ameongeza kuwa Tweet hiyo iende kwake, yaani mtu
akiandika tweet afanye kummention ili aione.
No comments:
Post a Comment