MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea
kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.
Akizungumza
kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa
sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye
tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
Diamond alisema hayo kwenye
mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika Runinga ya Clouds kwenye
Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku kituoni hapo.
DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa
nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi
yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui
niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya
kuachana kwetu na ilitokea tu.
“Naamini hilo jambo lilimuuma
sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema
(Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini
ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua
zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama
hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha
kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”
JACQUELINE WOLPER
Diamond
alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi
kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye alisema
ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.
PENNY SASA
Kwa
upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli
Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu
anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu kwa kweli ana
karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny ananiheshimu sana.
Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema hata kama
akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti,
tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu, hata kama
anafanya mambo yake ni kwa siri.”
No comments:
Post a Comment