MUME wa mwanamitindo maarufu hapa Bongo, Jacqueline Patrick, Abdullatif
Fundikira ‘Tiff”, aliyekuwa jela ya Gereza la Keko jijini Dar alikokuwa
akishikiliwa kwa tuhuma za kufanya biashara ya madawa ya kulevya,
amerudi uraiani baada ya kupata dhamana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu
makini, Tiff aliachiwa kwa dhamana Ijumaa iliyopita katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusota ‘lupango’ kwa takriban mwaka mmoja.
“Ni
kweli sasa hivi Tiff yuko mtaani, ametoka kwa dhamana ila kuhusiana na
suala la ndoa yake amesema haipo tena, anaangalia maisha yake,” kilidai
chanzo.
Katika kupata ukweli wa habari hii, mwandishi wetu alimpigia
simu Abdullatif lakini hakupokea ila Jack alipopatikana alikiri
zilipendwa wake huyo kuachiwa kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment