Show ya ufunguzi wa msimu mpya wa shindano la Big Brother Africa
itafanyika Jumapili hii, May 26 nchini Afrika Kusini.
Usiku huo
utawaonesha washiriki wote 28 watakaoanza safari ya miezi mitatu ya
kuzisaka dola laki tatu za msimu wa nane wa Big Brother Africa, The
Chase.
Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye ufunguzi huo ni pamoja na
STL wa Kenya, Don Jazzy, D’ Prince na Wande Coal kutoka Nigeria na
kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini.
Pia mchekeshaji wa Kenya Daniel Ndambuki, maarufu kama Churchill
atapanda kwenye stage kuwavunja mbavu watazamaji wa show hiyo katika
nchi 50 barani Afrika.
Show hiyo itaonekana live pia kupitia website ya
Big Brother,.
No comments:
Post a Comment