Rais Omari Al Bashir wa Sudan jana alilazimika kutoroka nchini Nigeria baada ya mikakati ya kumkamata kuvuja..
Rais Bashir aliyekuwa anahudhuria mkutano wa viongozi wa serikali za nchi za Muungano wa Afrika AU, kuhusu afya mjini Abuja amelezimika kuukatisha mkutano huo na kutoroka nchini humo jana Jumatatu kwa hofu ya kukamatwa
Rais huyo ameondoka nchini Nigeria ikiwa ni chini ya masaa 24 tangu awasili Nigeria
Makundi ya kutetea haki za kibinadam yameishutumu
vikali serikali ya Nigeria, kwa kumualika rais wa Sudan, Omal al-Bashir, nchini
Nigeria na siku ya jumapili walilitaka jeshi la nchi hiyo kumkamata rais huyo wa Sudan kabla hajaondoka.
Makundi hayo ya kutetea haki za kibinadam yamesema kuwa, ziara hiyo ni dharau kwa wahanga wa mzozo huo unaoendelea katika eneo la Darfur.
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa rais huyo kwa Sudan kwa tuhumu za kuhusika na mauaji ya halaiki.
No comments:
Post a Comment