Thursday, July 11, 2013

OMAR SYKES KUPEWA JINA LA MTAA MAREKANI‏

Na Swahili TV, Washington DC
Omar Sykes mwanafunzi  raia wa Tanzania aliyeuwawa  katika jiji la Washington, huenda akaenziwa kwa kupewa jina la mtaa ili kuweka kumbukumbu na ujumbe kwa wote walioathirika na  mauaji ya bunduki mitaani jijini Washington, Dc,  na Marekani kwa ujumla. Kama pendekezo hilo litapitishwa atakuwa mtanzania wa kwanza kupewa mtaa nchini Marekani.
Akiongea katika shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Omar Sykes, meya wa  jiji la Washington, mstahiki Vicent Gray,  alisema kuwa anatarajia kupendekeza katika kikao kijacho cha halimashauri ya jiji mwezi Septemba  kubadilisha mtaa wa…
Na Swahili TV, Washington DC
Omar Sykes mwanafunzi  raia wa Tanzania aliyeuwawa  katika jiji la Washington, huenda akaenziwa kwa kupewa jina la mtaa ili kuweka kumbukumbu na ujumbe kwa wote walioathirika na  mauaji ya bunduki mitaani jijini Washington, Dc,  na Marekani kwa ujumla. Kama pendekezo hilo litapitishwa atakuwa mtanzania wa kwanza kupewa mtaa nchini Marekani.
Akiongea katika shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Omar Sykes, meya wa  jiji la Washington, mstahiki Vicent Gray,  alisema kuwa anatarajia kupendekeza katika kikao kijacho cha halimashauri ya jiji mwezi Septemba  kubadilisha mtaa wa Fairmont  St, ambako mauti yalimkuta  ili uitwe Omar Sykes Street.
Meya Gray aliongeza  kusema kuwa  kitendo hicho kitakuwa ni ujumbe kwa nchi nzima ya Marekani  katika kuelezea ubaya wa ghasia za mauaji ya risasi mitaani. Marehemu Omar aliuwawa kwa risasi akiwa katika mazingira ya karibu na chuo kikuu anachosoma cha Howard.
Katika shughuli  hiyo ya kuuaga mwiili , Swahili TV ilifanikiwa kuona baadhi ya viongozi maarufu waliohudhuria  shughuli  hiyo kama Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Bwana Jandel Frazier.
Akiongea na Swahili TV, baba wa marehemu bwana Adam Sykes  ambaye naye alikuwepo katika shughuli hiyo, alisema ni heshima ya pekee kwa taifa kubwa kama hili kumuenzi  mwanae kwa kumpa jina la mtaa.
“Ni heshima ya aina gani kwa  taifa  kubwa kama hili kumuenzi  mwanangu  kwa kumpa mtaa”Alisema kwa majonzi huku akionesha furaha ya kupata heshima hiyo, bwana Sykes ambaye yeye na kaka Allyas Sykes waliwasili jumanne wiki hii nchini Marekani.
Swahili TV iliweza kuongea na  wananchi mbalimbali waliohudhuria  shughuli hiyo ambao  wengi walionyesha  hali ya majonzi   ya kifo cha kijana huyo,  mahojiano  ya Swahili TV na  baadhi ya viongozi wa serikali na Uongozi wa shule yatachapishwa na kuonyeshwa  katika Blog:  www.swahilitv.blogspot.com

No comments:

Post a Comment