Saturday, July 20, 2013

HIVI NDIVYO JESHI LA SERIKALI LILIVYOWAPA KICHAPO CHA MBWA MWIZI WAASI WA M23


 Goma -DRC.
WAKATI mapigano yakizidi kuwa makali kati ya wanajeshi wa DR Congo (FARDC) na kundi la waasi wa M23, wanajeshi wa DRC wako hatarani kushitakiwa kwa tuhuma za kuwatesa waasi na kunajisi maiti zao.
 
Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kosa la kukiuka haki za binadamu na sheria za Umoja wa Matifa (UN) inayokataza ukiukwaji wa haki za binadamu huku ukikataza watuhumiwa na mateka wa kivita kufanyiwa vitendo vyovyote vinavyo ashiria kukiuka haki zabinadamu badala yake mateka wote wanatakiwa kushtakiwa kwa muujibu wa sheria.

 Maiti ya muasi wa M23 ikinajisiwa na Askari wa Congo,baada ya kukamatwa, kuteswa hadi kufa katika mapigakano yanayoendelea maeneo ya Kivu na Goma nchini Congo.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon alisema kwamba, Umoja huo umeonyesha wasiwasi kuhusu taarifa ya kutokutendewa haki kwa wafungwa wa M23 na kunajisiwa kwa maiti ya wapiganaji wa M23 baada ya kukamatwa na vikosi vya silaha.

Alisema watuhumiwa wa M23 walifanyiwa vitendo vibaya na askari wa DRC mbele ya raia bila ya kuzingatia Sera ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu na kwamba watuhumiwa waliohusika katika matukio hayo watafanyiwa uchunguzi wa kina.

Wanajeshi wa DRC wakiinajisi maiiti ya muasi wa M23 baada ya kukamatwa na kupigwa hadi kufa mbele ya raia

Wanajeshi wa DRC wakiendeleza mateso makali kwa waasi wa kundi la M23 mpaka kifo kinapowafika wakiwa uraiani


Wanajeshi wa DRC wakiwa wamemfunga mpiganaji wa kundi la M23 nyuma ya gari na kumpitisha mitaani.


 Wanajeshi wa Congo wakimfunga askari wa kundi la M23 mbele ya raia baada ya kukamatwa

 
 Wanajeshi wa DRC wakimtembeza muasi wa kundi la M23 mitaani baada ya kukamatwa.

No comments:

Post a Comment