Friday, July 12, 2013

MADA MAUGO NA BENSON MWAKYEMBE KUZIPIGA NA MABONDIA WA RUSSIA

Bondia Mada Maugo.
TAARIFA KWA VYOMBO VY HABARI -MICHEZO
MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA -MADA MAUGO NA BENSON MWAKYEMBE (SONGEA) TAREHE 23-07-2913 WANATARAJIWA KUONDOKA JIJINI DAR-ES-SALAAM  KUELEKEA NCHINI RUSSIA KWA AJILI YA MAPAMBANO YAO DHIDI YA MABONDIA WA HUKO/KATIKA UKUMBI WA TRADE&INTERTEINMENT ULIOKO KATIKA MJI WA KASPIYSK, RUSSIA.
MADA MAUGO ATAZIPIGA NA MOVSUR YUSUPOV, WAKATI MWAKYEMBE ATAZPTWANGA NA APTI…
Bondia Mada Maugo.
TAARIFA KWA VYOMBO VY HABARI -MICHEZO
MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA -MADA MAUGO NA BENSON MWAKYEMBE (SONGEA) TAREHE 23-07-2913 WANATARAJIWA KUONDOKA JIJINI DAR-ES-SALAAM  KUELEKEA NCHINI RUSSIA KWA AJILI YA MAPAMBANO YAO DHIDI YA MABONDIA WA HUKO/KATIKA UKUMBI WA TRADE&INTERTEINMENT ULIOKO KATIKA MJI WA KASPIYSK, RUSSIA.
MADA MAUGO ATAZIPIGA NA MOVSUR YUSUPOV, WAKATI MWAKYEMBE ATAZPTWANGA NA APTI USTARKHANOV.
MABONDIA HAWA WATZIPIGA KATIKA UZITO WA SUPER -MIDDLE [kg 75] RAUNDI 8 KILA MMOJA.
REKODI ZA MPINZANI WA MADA MAUGO  NI MAPAMBAO MATATU AMBAYO AMESHINDA YOTE MOJA LIKIWA KWA KNOCK-OUT.
WAKATI MPINZANI WA MWAKYEMBE AMECHEZA MAPAMBANO MAWILI [2] NA AMESHINDA MOJA [1] NA KUPIGWA MOJA.
PAMOJA NA REKODI NDOGO WALIZONAZO WARUSI HAO ,HAIMAANISHI KWAMBA MABONDIA WETU WABWETEKE KWANI TARATIBU ZA MABONDIA WA NCHI KAMA RUSSIA NA NYINGINEZO ZA ULAYA NA ASSIA ,MABONDIA WAO HAWAWEZI KUANZA KUCHEZA NGUMI ZA KULIPWA MPAKA WAPITIE NGUMI ZA RIDHAA NA WAFIKIE KIWANGO CHA KUSHINDANA MASHINDANO YA OLIMPIKI.
HIVYO KWA MTAZAMO WANGU ,NI LAZIMA MABONDIA WETU WAJIANDAE VYA KUTOSHA ,KWANI WANAKENDA KUPAMBANA MAPAMBANO MAGUMU .
NA KATIKA KUTHIBITISHA KWAMBA MAPAMBANO NI MAGUMU HATA MIKATABA YAO INA MASHARTI MAGUMU, KIPENGELE NAMBA NANE [8] KATIKA MIKATABA YAO  KINAELEZA WAZIWAZI IWAPO BONDIA ATAPOTEZA PAMBANO KUTOKANA NA KUONYESHA KIWANGO CHA CHINI ,NA KAMA ATAPIGWA NA AKAONYESHA KUANGUKA KUTOKANA NA KUTOJIANDAA VIZURI ,NA IKAWA TUKIO LA KUANGUKA HUKO LIKO NDANI YA CHINI YA RAUNDI YA 5 BASI BONDIA HUYO ATALIPWA MALIPO KWA RAUNDI ALIZOZICHEZA TU.
HII IKIWA NA MAANA KWAMBA  HATA AKIPIGWA  RAUNDI YA KWANZA KUTOKANA NA KIWANGO  CHA CHINI ALICHOKIONESHA BASI ATALIPA MALIPO YA RAUNDI HIYO TU.
KWA MASHARTI HAYA AMBAYO MADA, NA MWAKYEMBE WAMEYAKUBALI NA KUSAINI MIKATABA HIYO NI WAZI MABONDIA WETU WANAKWENDA KUPAMBANA HASWA NA KWA JUHUDI ZOTE.
MASHARTI YA MIKATABA HII KWA KWELI INATULAZIMU HATA HUKU TANZANIA TUANZE KUYATUMIA ILI KUKOMESHA TABIA ZA MABONDIA WALAGHAI NA MATAPELI AMBAO HUJIANGUSHA ,AU KUACHA MAPAMBANO BILA SABABU ZA MSINGI  KWA LENGO LA ULAGHAI.
MASUALA YA KUOMBA VISA UBALOZI WA RUSSIA YAMEKAMILISHWA LEO HII 11-07-2013 NA GHARAMA ZIMESHALIPIWA ,NASI TPBO-LIMITED TUMESHATOWA KIBALI KWA MABONDIA HAO KUCHEZA RUSSIA ,NA WATAONGOZANA NA WAKALA WAO MKENYA THOMAS MUTUA ,ATAKAYEONDOKEA NCHINI KWAO KENYA NA WATAUNGANA PAMOJA -DUBAI
TUNAWATAKIA SAFARI NJEMA NA MCHEZO MZURI,NA MWENYEZI MUNGU AWARUDISHE SALAMA NCHINI TANZANIA.
                                                              IMELETWA KWENU NAMI;-
                                                    YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                          RAIS -Tanzania professional boxing organisation-limited
                              incorporeted under the companies ACT,2002 secton 5,Registration NO 95413

No comments:

Post a Comment