Saturday, July 20, 2013

MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTER AMWAGIWA TINDIKALI


Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Centre, Said Mohammed Saad ameripotiwa kumwagiwa tindikali jana usiku.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye Jamii Forum, Saad anadaiwa kuwa alimwagiwa Tindikali maeneo ya Msasani City Mall muda wa saa 2 usiku.
“Jamaa aliyefanya kitendo hicho alitoka mbio, mlinzi akamkimbiza lakini bahati mbaya akateleza na kuanguka na jamaa akawahi pikipiki na kutoweka eneo la tukio,” imesema taarifa hiyo.

“Said amelazwa Trauma (AMI) Hosp – Masaki. Kapata madhara macho yote mawili ila moja ndilo limeumia zaidi sehemu ya juu. Mwenyewe anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua na madaktari wanamhudumia. Polisi wanahaha kutafuta wahusika kwa nguvu kubwa na huenda akakamatwa mhusika mapema sana.”

No comments:

Post a Comment