Friday, July 12, 2013

Waarabu waliotaka kumnunua Kiemba wayeyuka

Amri Kiemba.

WAKATI sekeseke la usajili wa kiungo wa Simba, Amri Kiemba likionekana bado kutowekwa wazi, sasa imebainika kuwa dili hilo ni kama limefutika, kizuizi kikubwa kikiwa ni umri wa mchezaji husika.
Simba ilikuwa ikitoa taarifa kuwa kiungo huyo aliyewahi kuichezea Yanga, alikuwa akiwaniwa na timu kutoka Israel, Ureno na Raja Casablanca ya Morocco, huku ikidai kuwa inangoja dau likamilike ili aondoke nchini.
Taarifa za kuaminika ambazo Championi Ijumaa…
Amri Kiemba.
Na Khadija Mngwai
WAKATI sekeseke la usajili wa kiungo wa Simba, Amri Kiemba likionekana bado kutowekwa wazi, sasa imebainika kuwa dili hilo ni kama limefutika, kizuizi kikubwa kikiwa ni umri wa mchezaji husika.
Simba ilikuwa ikitoa taarifa kuwa kiungo huyo aliyewahi kuichezea Yanga, alikuwa akiwaniwa na timu kutoka Israel, Ureno na Raja Casablanca ya Morocco, huku ikidai kuwa inangoja dau likamilike ili aondoke nchini.
Taarifa za kuaminika ambazo Championi Ijumaa limezinasa ni kuwa, umri mkubwa wa Kiemba umekuwa kikwazo cha mchezaji huyo kupata dili kutoka kwenye klabu hizo zilizokuwa zikimuwania licha ya kuwa zimekiri kuwa kiwango chake kipo juu.
Alipoulizwa juu ya taarifa hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope, alisema imekuwa vigumu kwa mchezaji huyo kuweza kupata timu kirahisi kutokana na umri wake kumtupa mkono.
“Siyo rahisi kupata timu haraka kwa Kiemba kufuatia umri wake kuwa mkubwa, kwani kwa sasa ana miaka 30, hivyo kufanya klabu ziweze kusuasua katika suala zima la kumsajili.
“Kwa sasa bado tunaendelea na maongezi na klabu hizo na iwapo tutafikia makubaliano basi atakwenda,” alisema Hans Pope.
Hivi karibuni, Kiemba alisaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Simba kwa dau la shilingi milioni 35, licha ya kuwa Yanga nayo ilikuwa ikimuwania.

No comments:

Post a Comment