Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
Katibu
wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Nape Nnauye, amesema wanaopaswa kuulizwa jambo lolote linalohusu
uchaguzi wa udiwani wa kata nne uliofanyika Jumapili wiki iliyopita,
jijini Arusha, ni viongozi wa chama wa mkoa huo.
Nape alisema
hayo alipozungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, baada ya
kutakiwa kutoa maoni yake kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kuibuka mshindi katika kata zote nne.
“Waulize
wenyewe. Siwezi kuzungumzia issue (suala) ndogo. Unajua chama chetu
kimegawa majukumu. Kule kuna mwenyekiti wa mkoa, katibu pamoja na
wengineo,” alisema Nape.
Alipoulizwa
sababu za kutoa maoni katika chaguzi nyingine mara tu matokeo
yanapotangazwa, kama vile Jimbo la Igunga, Nape alisema uchaguzi huo
unahusu ubunge tofauti na udiwani.
Alisema
hata katika uchaguzi wa kata nyingine 22, alizungumza kwa kuwa ulikuwa
umehusisha kata mbalimbali nchini na siyo mkoa mmoja.
No comments:
Post a Comment