Thursday, March 20, 2014

TAARIFA ZAIDI YA SHABIKI WA YANGA ALIYEFIA UWANJANI KATIKA MECHI YA YANGA NA AZAM HAPO JANA

 
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, shabiki mmoja aliyedaiwa kuwa wa timu ya Yanga amefariki dunia jioni ya jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati timu hiyo ilipokuwa inacheza na timu ya Azam.
Shabiki huyo alizimia uwanjani mara baada ya Yanga kupata bao lake la kwanza lililofungwa na Didier Kavumbagu. Hata hivyo wasamaria wema walimbeba shabiki huyo na kisha kuwekwa kwenye machela na kupelekwa katika vyumba vya huduma ya kwanza.
Muda mchache baadae vipaza sauti vya Uwanja wa Taifa vilisikika vikitangaza kwamba kuna mtu amezimia na kama kuna ndugu au mtu yoyote wa karibu na mtu huyo ajitokeze. Taarifa zimeeleza kuwa mtu huyo amefariki akiwa katika chumba cha huduma ya kwanza na kupelekwa katika hospitali ya Temeke.
Katika mchezo huo ambao Yanga walianza kupata bao katika kipindi cha kwanza dakika ya 14. Hata hiyvo Azam ilipambana vikali na kurudisha bao katika kipindi cha pili ikiwa ni dakika ya 82 wakiwa wachezaji kumi baada ya Erasto Nyoni kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtukana muamuzi.

No comments:

Post a Comment