Sunday, March 2, 2014

Milipuko miwili yakumba mji moja Nigeria

 

Mji wa Maiduguri uliopo kazkazini mwa Nigeria umekumbwa na milipuko miwili, huku ripoti zikiarifu kwamba takriban watu 10 huenda wamepoteza maisha yao.
Mkaazi mmoja ameliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba mlipuko wa kwanza ulitokea katika eneo lililojaa watu huku wa pili ukilipuka wakati majirani walipokuwa wakiwasaidia waathiriwa.
Maafisa wa polisi wamesema kuwa watu wengi wamekwama chini ya vifusi.
Mji wa Maiduguri hutumiwa kama kambi ya wanajeshi wanaopigana na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Awali ripoti zimearifu kuwa kulikuwa na shambulizi la angani katika kijiji kimoja cha jimbo la Borno siku ya ijumaa.
Shahidi mmoja ameiambia BBC kwamba takriban raia 20 wamefariki.
Jeshi la Nigeria linadaiwa kuvilipua vijiji inavyoamini ni makao ya wanachama wa Boko Haram

No comments:

Post a Comment