Saturday, March 15, 2014

MTO MBEZI WAGEUKA TISHIO KWA WAKAZI WA GOBA

Wakazi wa pembezoni mwa Mto Mbezi wakivuka mto kuelekea upande wa pili.Wakazi wakiendelea kuvuka mto.
Mto Mbezi unaotembea kuanzia Mbezi Kimara kupitia Makongo juu B mpaka Goba kuelekea Kawe hadi baharini, umekuwa tishio kwa wakazi wa maeneo ya karibu na mto huo kwani hautabiriki na hata kipindi cha jua unajaa pasipo watu kujua mvua imenyesha wapi.
“Yaani mto huu ni tishio kubwa kwa wapita njia kwani unaweza kuwa eneo lako mvua haijanyesha ukajiamini kwa kupita lakini kama imenyesha eneo lingine ukashangaa maji yamejaa ambayo yanao uwezo wa kumeza mtu,  hili ni tatizo na mbaya zaidi unapanuliwa na wachimba mchanga” alisema mama Mmoja anayefahamika kwa jina la Mama Adelina.
Aidha wakazi wa huko wametoa kilio chao kwa serikali kuwatengenezea daraja kwa ajili ya kuvuka wakati wa mvua kwani ardhi ya huko kupita njia nyingine imekuwa haifai kabisa kwasababu ya mfinyanzi hasa wakati wa mvua tatizo ambalo ni la muda mrefu.

No comments:

Post a Comment