Thursday, March 13, 2014

69 wauawa na wafugaji Nigeria

 
Nigeria imeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia wasio na hatia
Takriban watu 69 wameuawa katika shambulizi dhidi ya kijiji kimoja katika jimbo la Katsina , Kaskazini Magharibi mwa Nigeria
Walioshuhudia shambulizi hilo walilaumu wafugaji wakisema kuwa washambuliaji waliingia kijijini mchana peupe wakiwa kwa pikipiki na kuanza kuwaua watu kiholela.
Mbunge mmoja anayewakilisha eneo hilo, Barrister Abdullahi Abbas Machika alisema kuwa watu 47 walizikwa hii leo katika kijiji kimoja katika jimbo la Katsina.
Duru kutoka katika hospitali ya Funtua,jimbo la Katsina, alisema kuwa angalau watu 15 wamelazwa hospitalini humo wakiwa na majeraha mabaya.
Wakazi wanasema kuwa hapakuwa na maafisa wa usalama, wakati wa shambulizi hilo tangu shambulizi lianze hapo jana.
Rais Goodluck Jonathan kwa sasa anazuru jimbo la Katsina kuzindua miradhi kadhaa ya maendeleo.
Mbunge anayewakilisha eneo hilo anadai kuwa maafisa wa usalama wanajishughulisha kumlinda Rais wakati raia wanauawa katika vijiji kadhaa.

No comments:

Post a Comment