Friday, March 14, 2014

MADAHA AKOMALIA NDOA NA MENEJA WAKE


Stori: Gladness Mallya

MWANA DADA kutoka kiwanda cha muziki na filamu Bongo, Baby Madaha ameonekana kukomalia kuolewa na meneja wake, Joe Kairuki huku akidai kuwa, mwanume huyo ni mume sahihi kwake.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Baby Madaha ‘Queen of Swaga’ alisema kutokana na uhusiano wake na Joe kuelekea kwenye ndoa, mara nyingi amekuwa akila bata zake nchini Kenya ambako ndiko mchumba wake huyo anakotokea.

“Mimi sijui kwamba ni mume wa mtu kwani sijawahi kumuona huyo mwanamke ila ninachokijua Joe ana mtoto na hajafunga ndoa na aliyezaa naye tena wanaishi nchi tofauti kwa hiyo sioni shida kuwa naye na mipango ya ndoa ipo,” alisema msanii huyo.

No comments:

Post a Comment