Friday, March 14, 2014

Mashambulizi makali yatokea Maiduguri

Polisi wakidhibiti ulinzi katika barabara za Maiduguri
Taarifa za hivi punde zinasema kuwa kumetokea mashambulizi makali ya ufyatulianaji risasi mjini Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wakazi wa mji huo wanasema kuwa walisikia ufyatuaji wa risasi na milipuko kwa karibu saa mbili nyakati za Asubuhi.
Inaarifiwa tukio hili limejiri wakati, wa kile kinachoshukiwa kuwa shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi lililofanywa na wapiganaji wa Boko Haram.
Maelfu ya watu wameuawa nchini Nigeria katika kipindi cha miaka mitano tangu kundi la Boko Haram lilipoanza vita.
Ghasia hizi zimekithiri katika miezi michache iliyopita, licha ya juhudi za maafisa wa usalama kuzidhibiti usalama na kutangazwa kwa hali ya tahadhari katika majimbo matatu.

No comments:

Post a Comment