Friday, May 31, 2013

Diamond Platnumz "Jokate Nisamehe"

MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku kituoni hapo.

DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.

“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”

JACQUELINE WOLPER
Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline  Wolper ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.

PENNY SASA
Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu, hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”

KIJANA ANUSURIKA KUFA BAADA YA VIBAKA KUMCHOMA MOTO HUKO MKOANI LINDI


Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ismai Mayoba(31) anayefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Manispaa ya Lindi amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto. 

Kwa sasa kijana huyo amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.

Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mtu  mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.


Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndugu Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie Moto huku akijua ni kosa kisheria.

Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo

ZANZIBAR YAPIGA MARUFUKU NDOA ZA JINSIA MOJA.....UKINASWA IMEKULA KWAKO ( MIAKA 30 JELA )



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu. 


Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.

Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa kunukuu.

BUNGENI: Vurugu zasababisha Bunge kuahirishwa hadi jioni.

Kufuatia hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha cuf kuwa ni chama cha kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita chadema ni wehu, wahuni, wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha cuf...

Mbunge huyo wa CUF ameomba spika achukue hatua za dhidi ya chadema asipofanya hivyo cuf watachukua hatua dhidi ya Chadema na bunge..

Kumetokea vurugu bungeni ambapo spika ameliahirisha bunge hadi jioni.

Hiki ni Kipande cha hutuba hiyo ambacho nimekitoa Jamii Forums:
"Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”. Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata mrengo huo.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo "

NESI ANASWA KATIKA JARIBIO LA KUMTOA MIMBA MWANAFUNZI....

Mwanafunzi akiwa kitandani tayari kwa kutolewa mimba

MUUGUZI wa kike, Violet Shoo, mkazi wa jijini Dar ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni, Ilala baada ya kunaswa katika jaribio la kutaka kumchoropoa ujauzito msichana mmoja aliyepandikizwa kama mwanafunzi kwa mtego makini ulioratibiwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’

Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita, saa 11 jioni kwenye zahanati iliyopo Tabata Matumbi, jijini Dar es Salaam. 
 Nesi akidhibitiwa na polisi...

Muuguzi huyo alikutwa ndani ya zahanati hiyo akiwa na zana mbalimbali zinazodaiwa ni za kutolea mimba huku msichana huyo akiwa juu ya kitanda, tayari kwa kufanyiwa zoezi hilo haramu.
 
Awali, Ijumaa ya Mei 23, mwaka huu baadhi ya wakazi wa eneo hilo walitutumia ujumbe  wakimlalamikia muuguzi huyo kwamba amekubuhu katika matukio ya utoaji mimba hivyo wakaomba ikiwezekana OFM imuandalie mtego wa kumnasa ili kukomesha kitendo hicho.
 
“…huyu nesi amekuwa akiwatoa watoto wetu mimba, kwa siku anaweza kutoa hadi nne, sisi wazazi tumechoshwa, tunaomba mje. Anaitwa Violet…” ilisomeka sehemu ya meseji hiyo huku ikielekeza zahanati anapopatikana.
Nesi akiwa chini ya ulinzi....
Baada ya malalamiko hayo, kikosi cha upelelezi cha OFM chenye wasichana wawili kilikwenda kwenye zahanati hiyo na kukutana uso kwa uso na muuguzi huyo ambapo msichana mmoja aliomba kutolewa mimba na nesi huyo ambapo aliambiwa ni shilingi 50,000.

Kikosi kiliondoka kwa kumwambia muuguzi huyo kwamba wanafuata fedha mahali na wangerejea jioni wakiwa na  pesa mkononi. 

Timu ya waandishi wetu wa habari  pamoja na Jeshi la Polisi waliweka mtego baada ya wakazi wa maeneo iliyopo zahanati hiyo kulalamika juu ya kukithiri vitendo vya utoaji mimba vinavyofanywa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.
 
Wakazi wa maeneo hayo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe , walidai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupiga simu katika chumba cha habari kuwa idadi kubwa ya wanawake wanatolewa mimba kwa siku katika zahanati hiyo bubu ambayo haina jina wala hadhi ya kutoa huduma.
 
Baada ya hapo, waandishi hao wa kike walirejea ofisini na kutoa taarifa kwa mabosi wao ambapo timu kamili ilipangwa.

Mkuu wa timu hiyo alianzia Kituo cha Polisi Buguruni ambapo alitoa taarifa kuhusu malalamiko ya wakazi wa eneo hilo na jinsi muuguzi huyo alivyofikia hatua ya kutaka alipwe elfu hamsini ili kukamilisha zoezi.
 
Afande mkuu akatoa maagizo kwa watu wa chini yake watatu, akiwemo askari wa kike mmoja kwa ajili ya kwenda kumnasa nesi huyo.

Msichana aliyepandikizwa kutolewa mimba akiwa na mwenzake walitangulia kufika kwenye zahanati hiyo lakini hawakumkuta muuguzi huyo. 

Mfanyakazi mmoja wa zahanati hiyo alimweleza ‘mtolewa mimba’ kwamba nesi huyo alikwenda kusuka na tayari ameshawasiliana naye hivyo wasubiri.

Saa kumi na nusu, muuguzi huyo aliwasili kwa ajili ya kazi hiyo huku mawasiliano yakifanyika kati ya mtolewa mimba na waandishi waliokuwa jirani na eneo la tukio.
 
Ndani ya dakika kumi, waandishi na polisi waliitwa eneo la tukio wakijulishwa kwamba ‘mjamzito’ huyo ameshavua nguo tayari kwa kazi ya kuchoropolewa mimba.

Kikosi kazi kilivamia zahanati hiyo ambapo walikuta zoezi linaendelea. Polisi wenye ujuzi wa kazi za kunasa matukio walimtia mbaroni muuguzi huyo akiwa na zana za shughuli huku wakimwambia kosa lake.

Vifaa vilivyotumika....
 
Wakati huo, mjamzito alikuwa yupo kitandani katika maandalizi ya kutolewa mimba.

Wananchi waliokuwepo eneo la tukio wakati mtanange ukiendelea, walionekana kufurahishwa na kitendo cha kukamatwa kwa muuguzi huyo huku wakidai walikuwa wamechoka naye kutokana na vitendo vyake vya kutoa mimba hadi kwa wanafunzi.
 
“Tumekuwa tukijitahidi kutoa taarifa katika vyombo vya dola ikiwemo ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu lakini hakuna hatua zozote zilizokuwa zikichukuliwa, ndiyo maana tukaamua kuwasiliana na nyie waandishi wa habari ili mtusaidie,’’ alisema mkazi mmoja bila kutaja jina lake.

Muuguzi huyo alipoulizwa kwa nini amekuwa akijihusisha na vitendo hivyo, alikaa kimya.

Mjumbe wa Nyumba Kumi, Shina Namba 26, Tawi la Mandela, Rogasian Chadima alikuwepo katika eneo la tukio baada ya kufuatwa na polisi, naye aliahidi kufuatilia suala hilo akisema kwanza hakujua kama kuna zahanati katika eneo lake.

Safari ya kwenda polisi kwa mahojiano ilianza hapo huku muuguzi huyo akiwa na ‘ushahidi’ wake mkononi. Muda mwingi alionekana asiyeamini macho yake kwa kile kilichomtokea.

GPL

VIDEO: HUU NDO UCHAFU UNAOTENDEKA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA

Hii ni video inayoonesha  uchafu  unaotendeka  ndani ya jumba la Big Brother Africa....
 
Nashindwa  kuusimulia, ila jionee mwenywe  katika  video  hiyo.....

Wednesday, May 29, 2013

AIBU YA BIG BROTHER: VIDEO ZA MAPENZI ZAANZA KUONEKANA KATIKA NYUMBA ANAYOIONGOZA FEZA KESSY WA TANZANIA


Ikiwa ni usiku wa pili (usiku wa kuamkia leo)katika reality show ndani ya jumba la Big Brother Africa mwaka huu lilipewa jina la ‘The chace’ mambo mengi mapya yameanza kuonekana kwa washiriki ambao wameanza kufahamiana.
 
Katika hali ambayo mara nyingi haikwepeki hasa wanapokutana wanawake warembo na wanaume watanashati, scene za mapenzi zimeanza kuonekana katika Diamond house inayoongozwa na mtanzania Fezza Kessy (Head of house) ....

‘Bolt’ , mshiriki kutoka Sierra Leone na Betty ambae ni mshiriki kutoka Ethiopia walipata nafasi ya kufahamiana zaidi na kuvuka mstari wa urafiki wa kawaida wakati washiriki wengine wakiwa wamelala  ndani ya jumba la Kessy
Betty na Bolt..

Betty ambae yuko nominated pasipo yeye kufahamu, sasa yeye na Bolt ndio waliothibitishwa kuwa couple ya kwanza, japo hatima ya mahusiano yao huenda ikawa hatarini kwa kuwa jumapili hii kura za watazamaji zitaamua hatima ya Betty kuendelea kuwa katika jumba hilo au kurudi Ethiopia.

Ilala yatoa siku saba ghorofa litoke

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetoa notisi ya siku saba kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na mmiliki wa jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri kulibomoa ndani ya kipindi hicho.
Ghorofa hilo linalomikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Ally Raza linabomolewa baada ya kuanguka kwa jengo pacha la aina hiyo Machi 29 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 36, kujeruhi 18 na uharibifu wa mali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema kuwa, notisi hiyo imeanza Mei 27 hadi Juni 3 mwaka huu.
“Tayari tumewakabidhi NHC na Ally Raza mmiliki wa jengo la ghorofa 16 notisi ya siku saba ya kumtaka kubomoa jengo hilo ndani ya siku saba na asipotekeleza hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa,” alisema Silaa.
‘‘Kwa mujibu wa sheria ya mipango miji, mmiliki halali wa kiwanja hicho ni NHC, na wao ndiyo waliomuuzia Raza eneo hilo ili aweze kujenga ghorofa’’ alisema.
Kwa mujibu wa Silaa, kutokana na ramani iliyotolewa na mipango miji, maeneo yote ya Kisutu yanatakiwa kujengwa ghorofa 10 na si vinginevyo, lakini cha kushangaza, Mhandisi kutoka Bodi ya Wahandisi, msanifu majengo na makandarasi wameweza kusimamia ujenzi wa ghorofa 16 kinyume na taratibu.
Alisema, kitendo cha Manispaa hiyo kuingia kwenye lawama ambazo pia zinawahusu NHC, wahandisi, wasanifu majengo na wakandarasi kwa kuidhinisha ujenzi wa ghorofa 16 wakati eneo hilo linaruhusiwa kujengwa ghorofa 10 ni sawa na kutowatendea haki.Alisema kutokana na hali hiyo kila mmoja anapaswa kuwajibika kulingana na nafasi yake ili siku nyingine waweze kufuata sheria na taratibu zilizopo wakati wa kuidhinisha majengo nchini.
Alisema, kutokana na hali hiyo wameiomba tume iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza ghorofa hiyo kutoa ripoti mapema ili waweze kuijadili na kutoa mapendekezo yao.
Hali hiyo inatokewa wakati Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka juzi wakati wa kuwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake, alizitaka Manispaa ya Ilala, NHC na mmiliki wa ghorofa hilo kulibomoa ghorofa hilo.

P-Funk Atoa Ujumbe Mzito Kuhusu Kifo cha Mangwear Ailaumu Clouds Fm



Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.

Imezibitishwa Mangwear Kafariki kwa Kujioverdose Cocaine na Crack:Soma Report ya Doctor Hapa

The Medical report from Helen Joseph hospital,Dr Shirley Radcliffe  confirming that albert Mangwairdied from “alcohol toxicity” after drinking toomuch,Over-exhaustion and drugs overdose....The inquest heard that Albert 28, collapsed in the his friends home had been more thanfive-times the legal S.A drink-drive limit with 416mgof alcohol per 100 millilitres of blood in hissystem....Radcliffe described thereasons for ICU admission included hypoxemia and one of his friend found “two empty vodka bottles[found] on the Car” and he hadbeen suffering from the eating disorder Bulimiafor several months before his death and endless partying session with little or no resting...sample taken from his stomach showed poly-drug cocktail and he overdosed Heroin,Cocaine 'crack' and cannabis 0.08gms was also found in his blood...and his death was caused by massive heart attack and respiratory failure followed by sudden Heart stop...and end up dead within seconds! R.I.P Mangwear!

Monday, May 27, 2013

LWAKATARE AKWAMA TENA KUPATA DHAMANA, KESI YA JAYDEE YARUSHWA MPAKA JUNE 13.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare na mwenziye Ludovick Joseph wamekwama tena leo Jumatatu, Mei 27 kupata dhamana baada ya Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu, Sundi Fimbo kueleza kuwa Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Aloyce Katemana, bado yupo likizo tangu wiki tatu zilizopita.
  
Watuhumiwa wanakabiliwa na shitaka la kupanga njama za kumnywesha sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.

Lady Jay Dee akiwa na mumewe Gardner Habash wakisuburi kesi kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kindondoni leo asubuhi saa tatu. 
------------------
Mwanamuziki Judith Wambura-Habash --Lady Jay Dee-- alifika katika mahakama ya Kinondoni leo kama ilivyotakiwa kwa mashitaka aliyofunguliwa hapo. Baadaye amefahamisha kuwa ameambiwa ardui tarehe 13 Juni 2013.
Kesi imetajwa tena tar 13 June 2013. Saa 5 asub.

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka

Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.

Fezza Kessy Awa Mtanzania wa Pili Kuingia Nyumba ya Big Brother Africa

Baada ya Kuwa na Tetesi kuwa Fezza Kessy Atakuwa ni mmoja wa wakilishi wa Tanzania Big Brother Africa ...leo hii Amekuwa ni Mmoja kati ya Watanzania Wawili Wanao Iwakilisha Tanzania katika Jengo Hilo....So Tuna Wawakilishi Wawili Nando na Fezza Kessy...
 

Matapeli wa kwenye mtandao wamuandama Wolper! Soma hapa kilichomtokea leo na alichosema kuhusu Facebook.

Matapeli wa kwenye mtandao wamuandama Wolper! Soma hapa kilichomtokea leo na alichosema kuhusu Facebook.

Katika kile kinachoonekana ni mwendelezo wa matapeli wa mjini kutumia majina ya waigizaji maarufu nchini kutapeli watu kwa njia ya mtandao, dhahama hii sasa imemkuta mwanadada Jacqueline wolper baada ya watu wanaoaminika kuwa ni matapeli kutumia jina lake kujipatia fedha na vitu vingine kiudanganyifu.

Akizungumza kwa simu na tovuti ya bongomovies.com mwanadada Jacqueline wolper  alisema matapeli hawa sasa wameamua kutumia mtandao wa instagram na mtandao mwingine wa kijamii uitwao badoo kwa jina la “wolper gambe25” katika kutapeli watu kwa kuwaomba hela au michango mbalimbali kupitia account hizo feki

“Leo nilikuwa naenda saluni, baada ya kufika tuu, yule dada wa saluni akaanza kunilalamikia kuwa mbona sijaenda kuchukua viatu nilivyomuagiza pamoja na hela? Nikawa sijui cha kumwambia maana sikumuagiza viatu na wala sijampigia simu kumwambia anitumie hela, ndipo aliponionesha huo ujumbe kwenye simu yake na ndio nikagundua hizo account feki za hao watu wanaoutumia jina langu kutapeli watu” Alisema Jack.

“Mimi sipo facebook na wala sitarajii kujiunga, nawaomba sana mashabiki wangu wajue hilo. Natumia mtandao wa instagram kwa jina la wolpergambe au jacklinewolperjacklinewolper.” Alisisitza Wolper

Pia alisema kuwa amendundua leo kuna mtu mwingine anayetumia jina lake kuomba watu wamchangie kuhusu kampeni inayoitwa “Zinduka” na amewataka sana mashabiki wake wasije wakafanya hivyo kwani mtu huyo ni mwizi na analengo la kumchafulia jina lake.

Thursday, May 23, 2013

Kikwete: Hata kama Mtu anaechochea Wananchi Ana Pembe Tutayakata

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani mh Jakaya Kikwete leo akihutubia ktk Mkutano wa CCM mkoani Dodoma huku akionekana mwenye hasira, amesema kua Serikali haipo tayari kuwavumilia wale wote wanachochea wananchi kufanya Vurugu baada ya Waziri wa Nishati na Madini kuwasilisha hotuba yake leo.

Alisema kua wapo watu Viongozi wanaochochea kwa Maslahi ya kisiasa na kwamba watahakikisha wote wanakamatwa iwe wapo ndani au nje ya nchi na kuwafikisha ktk vyombo vya Sheria.
Akiongea kwa hasira alisema kua Hata kama anaechochoe Wananchi kufanya Vurugu Ana PEMBE watamkamata na kumkata hizo Pembe.

Source: TBC1 TAARIFA YA HABARI.

Afande'Edward'aliyekamatwa na magunia18 ya bangi Himo ametoroka mikononi mwa polisi!

Alikua akipelekwa nyumbani kwake kwa upekuzi zaidi,Inspector Isaac aliyekua kiongozi wa askari wakimsindikiza ashikiliwa kwa uchunguzi zaidi,mwenzie pc George afikishwa mahakamani leo.

AJALI MBAYA YA MAGARI MATATU CHANG'OMBE JIJINI DAR



Ajali mbaya iliyohusisha magari matatu imetokea katika barabara ya Chang’ombe jijini Dar es salaam na kusababisha msongamano mkubwa wa magari; na watu kuchota mafuta yanayomwagika kutoka kwenye Lori hilo.

MASHABIKI NCHINI KENYA WAMZOMEA MR NICE HUKU WAKIMUITA MAC MUGA



Mtandao wa ghafla kutoka Kenya umeripoti kuwa, msanii Mr Nice, amejikuta akizomewa na umati wa watu waliokuwa katika Club moja inayoitwa Iclub, ambapo wachekeshaji Fred Omondi na Mc Antonio hufanya show zao pale kila siku za jumapili.
inasemekana Mr Nice alikua ameenda pale kwa ajili ya kula good time tu, na kufurahisha nafsi yake, lakini matokeo yake hayakua kama alivyotarajia. pale mchekeshaji Mc Antonio alipomuona Mr Nice katikati ya watu, na kwakuwa ni mtu maarufu, Mc akamuambia awapungie mikono watu waliokuwepo pale, lakini Mr Nice hakufanya hivyo wala kusimama akidaikuwa yeye ni msanii ambae amesainiwa na Mc huyo hawezi kumlipa yeye, na akipanda jukwaani hapo atashitakiwa na magement yake.
inasemekana mashabiki walipata kichekesho kipya pale ambapo Mr Nice aliponyanyuka na kusema " Hamnilipi mimi nikipanda hapa kwenye jukwaa, nitashtakiwa mimi" baada ya kusema maneno hayo mashabiki walianza kumzomea huku wakipiga kelele wakisema Mac "Muga" wimbo wa Ally Kiba, ambao unasemekana kuwa unamdiss yeye. na dj hakuwa na hiyana aliupiga wimbo huo maana mashabiki waliutaka

Wednesday, May 22, 2013

WEZI WAANZA TENA BUKOBA

baada ya baadhi ya wana nchi kuwa wana ozea jera kwa makosa ya kushiliki kupiga wezi na kuwauwa sasa wametengeneza hari ya uoga inayo wafanya majizi kuwa huru katika kufanya kazi yao hali inayo wafanya baadhi ya wananchi kulia na kusaga meno