Tuesday, July 9, 2013

MANDLA: MJUKUU WA MANDELA MWENYE VITUKO VINGI

Mandla Mandela.
Mwandishi Wetu na Mitandao

MJUKUU  wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aitwaye Mandla Mandela amekuwa na vituko vingi na kushangaza dunia.

Mandla akiwa na mke wake wa pili Anais Grimaud.
Licha ya kuachana na wake zake wawili, mmoja akimtuhumu kutembea na kaka yake, Mandla amekumbwa na kashfa baada ya kushindwa kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yake na ndugu zake akidaiwa kufukua makaburi ya watoto wa Mandela na kwenda kuwazika upya katika Kijiji cha Mvezo, umbali wa kilomita 22 kutoka Qunu…
Mandla Mandela.
Mwandishi Wetu na Mitandao
MJUKUU  wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aitwaye Mandla Mandela amekuwa na vituko vingi na kushangaza dunia.

Mandla akiwa na mke wake wa pili Anais Grimaud.
Licha ya kuachana na wake zake wawili, mmoja akimtuhumu kutembea na kaka yake, Mandla amekumbwa na kashfa baada ya kushindwa kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yake na ndugu zake akidaiwa kufukua makaburi ya watoto wa Mandela na kwenda kuwazika upya katika Kijiji cha Mvezo, umbali wa kilomita 22 kutoka Qunu alikofukua.
Mgogoro huo ulihusu maiti za wanawe Mandela watatu Madiba, Makgatho na Makaziwe Mandela ambao Mandla aliwazika karibu na nyumbani kwake zaidi ya miaka miwili iliyopita bila kuwa na sababu za msingi.
Mahakama kuu nchini Afrika Kusini iliamua kuwa maiti hao lazima warejeshwe katika makaburi yao ya awali ya Qunu Jumatano iliyopita, sehemu ambayo Mandela, ambaye anaumwa sana hospitalini anataka kuzikwa akifa. Mandla aliyetawazwa kuwa kiongozi wa kabila lao na babu yake, sasa anapinga vikali amri hiyo.
Tayari Mandla ana mgogoro mwingine na familia kwa kuuza hati miliki ya matangazo ya mazishi ya babu yake ambapo inadaiwa ‘amelamba’ Randi 3,000,000 (Zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 615) kutoka Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) japokuwa kulikuwa na habari kwamba alishavuta Randi 2,000,000 (zaidi ya shilingi milioni 326) kutoka kwa Shirika la habari la Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment