Tuesday, July 9, 2013

AMUUZA MWANAE WA KUMZAA KWENYE FACEBOOK


RIYADHI, Saudi Arabia
JAMAA mmoja amemuuza mwanae wa kumzaa kutokana na matatizo ya kifedha aliyonayo.
Saud bin Nasser Al Shahry, raia wa Saudia Arabia aliweka picha ya mwanae huyo wa kiume kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii ‘Facebook’ akimnadi kwa bei ya dola milioni 20.
Baba huyo alidai kuwa kitendo cha kumuuza mwanae ndiyo njia pekee ya kuondokana na maisha ya kimaskini aliyokuwa nayo kutokana na madeni.

Mahakama ya nchini humo ilifunga biashara yake ya kukusanya madeni isiyo rasmi aliyokuwa akiifanya ili kujikimu kimaisha, hivyo alibaki hana mbele wala nyuma hivyo kushindwa kumudu gharama za maisha.
‘Mfanyabishara’ huyo alidai aliomba Serikali imsaidie fedha, lakini ilimkatalia kwa kuwa umri wake ni zaidi ya miaka 35 ambao ni mdogo. Alisema akifanikiwa atatumia fedha hizo kumtunza mke wake na mwanae mwingine wa kike.

No comments:

Post a Comment