Thursday, February 20, 2014

Wanahabari kufikishwa mahakamani Misri

 
Waandishi habari waliokamatwa Misri
Waandishi habari 20 wakiwemo 4 wa kigeni wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo mjini Cairo, Misri.
Wanne hao wanakabiliwa na makosa ikiwemo, kujihusisha na shirika la kigaidi na kuhatarisha usalama wa kitaifa.
Washitakiwa wanane miongoni mwao mhariri mkuu wa ofisi ya shirika la habari la Al Jazeera Misri Mohamed Adel Fahmy na aliyekuwa mwandishi wa BBC Peter Greste pamoja na raia mmoja wa Australia watafikishwa kizimbani.
Kesi dhidi ya waandishi wengine wakiwemo waandishi wawili waingereza, itakasikilizwa bila ya wao kuwa mahakamani.
Shirika la habari la Al-Jazeera linasema kuwa tisa pekee ya wale waliokamatwa ni wafanyakazi wake na walikuwa wanaripoti tu kuhusu matukio nchini Misri walipokamatwa
Aidha shirika hilo limetaja madai dhidi ya wanahabari hao kama ya kipuuzi na yasiyo na msingi na pia limekanusha kusaidia vuguvugu na Muslim Brotherhood ambalo limetajwa kuwa kundi la kigaidi baada ya kuondolewa mamlakani kwa rais wa zamani Mohammed Morsi
Wizara ya mambo ya kigeni Marekani imeituhumu serikali ya Misri kwa kuwalenga waandishi wa habari kwa kuwasingizia mashitaka yasiofaa waandishi hao na kupuuza haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment