Monday, February 24, 2014

PIGO LA PILI KWA LOWASSA, BADO LA TATU NA LA MWISHO


"Bwana Lowassa,

Nikupe pole nyingine baada ya ile ya juzi kati kukueleza vichomi ulivyotegeshewa na ambavyo vimeanza kukuchinjia baharini tena kuleeeee Nungwiiiii, Naam umepigwa kufuli kutojishughulisha na siasa za uongozi mpaka mwezi wa pili mwakani,

Sasa ulijiandaa kuteka siasa kwamgongo wa katiba mpya, ikawa usiku ikawa mchana, naaam leo Chenge kakulamba chenga ya kisigino, ndio kakutelekeza, tena alfajiri tu.

Chenge kaiona pepo japo ni ya masika tu na kaniki haifuliwi kwa maji ya mvua.

Chenge hatunae tena kwenye anga la ukuu wa katiba mpya, sasa ni yuleyule aliyekupeleka kibla mnamo 2007, si mwingine ni Samwel Sitta mbabe wako kutoka CCJ.

Wayajua mapigo mawili yaliyo mbele yako??

Haya tutaftane..."

By Yericko Nyerere From JF

No comments:

Post a Comment