Friday, February 28, 2014

Mchangie Mtoto Huyu Anayeteseka na Majeraha ya Moto..!

Salome Kiegu (Mama mkubwa wa mtoto) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya akiwa amempakata mtoto Adolotea Njavike (1.4) aliyepata ajali ya moto akiwa na mamayake na kusababisha viungo vyake kuungana kwa sasa.

MTOTO Adolotea Njavike (1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na kichwa na kiwiliwili kuungana baada ya kupata ajali ya moto akiwa na mama yake mzazi.
Akizungumzia mkasa huo mamamkubwa wa mtoto Salome mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya alisema mtoto huyo alipata ajali ya moto katika mazingira ya kutatanisha kwani waliangukia kwenye moto yeye na mama yake hivyo mtoto huyo kujeruhiwa vibaya. Alisema tukio hilo lilitokea Agosti, 2013 lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida wakati wa kula na hata kucheza na wenzake.
Alisema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute shilingi 100,000 ili mtoto wake aweze kutibiwa.
Alisema kuwa baada ya muda wataalamu walimwambia asubiri wazungu kutoka Ulaya ambao baada ya kusubiri kwa muda wazungu hao walifika na kumcheki mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.
Aidha kutokana na kuambiwa hivyo mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka mtoto wake kwa matibabu kwani hana uwezo wa kugharamia safari hadi Dar es Salaam pamoja na matibabu. Alisema kwa mujibu wa waliomshauri kwenda kwenye matibabu anahitaji zaidi ya shs milioni 2 ili ziweze kumsafirisha na kugharamia matibabu pamoja na huduma za kawaida akiwa kwenye matibabu ya mwanaye.
Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment