Friday, February 21, 2014

FAMILIA YAISHI CHOONI BAADA YA PAA LA NYUMBA YAO KUEZULIWA NA UPEPO

 
Aziza Mohamed(55)akiwa na mjukuu wake katika choo ambacho hivi sasa wamekigeuza kuwa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua nyumba yake wilayani Hai.FAMILIA moja ya watu watatu akiwemo mtoto wa umri wa miaka saba imelazimika kuhamishia makazi chooni baada ya paa la nyumba waliyokuwa wakiishi kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita katika wilaya ya Hai.Familia hiyo ya Aziza Mohamed (55) mwanae wa kiume, Sikujua Aloyce(40) na mjukuu wake wakazi wa kitongoji cha Kijiweni kijiji cha Mijongweni kata ya Machame Weruweru imekuwa ikiishi kwa zaidi ya siku 14 katika choo hicho ambacho paa lake lilisalimika wakati mvua hiyo ikinyesha.

No comments:

Post a Comment