Thursday, June 20, 2013

LWAKATARE APOKELEWA KWA SHANGWE, AFANYA MKUTANO MJINI BUKOBA

Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliofika uwanja wa ndege kumpokea Lwakatare.
Umati wa watu uliohudhuria mkutano wa Lwakatare.
Lwakatare…
Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliofika uwanja wa ndege kumpokea Lwakatare.
Umati wa watu uliohudhuria mkutano wa Lwakatare.
Lwakatare akisalimiana na mmoja wa wafuasi wa Chadema.
Umati wa watu ukifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Muganyizi Lwakatare, jana alipokelewa kwa shangwe na wafuasi wa chama hicho katika Uwanja wa Ndege mjini Bukoba. Baadaye Lwakatare alifanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara mkoani hapo katika Uwanja wa Uhuru baada ya kutoka rumande kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili ya kutaka kumwekea sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msaki. Maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba walihudhuria mkutano huo ambapo Lwakatare alieleza mambo mengi ambayo amejifunza akiwa rumande.

No comments:

Post a Comment