Wednesday, June 19, 2013

Brandts, Liewig wataja kilichoimaliza Stars

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig.
Na Khatimu Naheka

KUFUATIA kipigo ilichopata Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast, Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts na aliyekuwa kocha wa Simba, Patrick Liewig wametoa siri ya matokeo hayo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts
Kauli hiyo ya makocha hao, inakuja kufuatia Stars mwishoni mwa wiki iliyopita kukubali kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa timu…
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig.
Na Khatimu Naheka
KUFUATIA kipigo ilichopata Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast, Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts na aliyekuwa kocha wa Simba, Patrick Liewig wametoa siri ya matokeo hayo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts
Kauli hiyo ya makocha hao, inakuja kufuatia Stars mwishoni mwa wiki iliyopita kukubali kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa timu hiyo.
Huo ulikuwa mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani zitakazofanyika nchini Brazil.
Akizungumza na Championi Jumatano, Brandts alisema licha ya kuonyesha kutokubaliana na penalti waliyopewa Ivory Coast, iliyotolewa na mwamuzi Mehdi Abid kutoka Algeria, beki wa Stars, Erasto Nyoni, ndiye aliyewapa ushindi Tembo hao kutokana na kushindwa kuhimili mbinu za kiungo, Gervinho.
“Kuna tukio kabla ya kutoa penalti ile ambalo ndilo lilikuwa halisi kwa mwamuzi kusema beki alimsukuma mchezaji wa Ivory Coast. Penalti ile iliwapa tabu sana Tanzania kwani walipewa kazi ya kufikiria kurudisha bao.
“Lakini sidhani kama pale alikuwa sahihi, nafikiri alidanganywa, ukiachana na hilo nimeona jinsi beki namba mbili (Nyoni) alivyokuwa katika wakati mgumu, sikujua kwa nini hakumfanyia mabadiliko mapema,” alisema Brandts.
Wakati Brandts akiyasema hayo, Liewig aliipongeza timu hiyo kwa kuonyesha ujasiri wa kupambana na Ivory Coast, lakini akapinga juu ya mfumo wa ukabaji wa Stars ambao uliwapa nafasi viungo washambuliaji wa Tembo hao nafasi kubwa ya kuwasumbua.
“Inawezekana mabeki walizidiwa lakini nililoona mimi ni kwamba, ukiangalia Stars ilikuwa inashindwa kuwakaba viungo wa Ivory Coast, ukiacha suala la kuzalisha penalti.
“Gervinho alitokea mbali akiambaa na mpira akiwapita watu watatu, sidhani hapo kama utapongeza timu ilikaba vizuri, ni lazima kocha alifanyie kazi mapema,” alisema Liewig.

No comments:

Post a Comment