Wednesday, June 19, 2013

BOSI WA GERVINHO AIPA YANGA SC KIFAA

Na Saleh Ally

YANGA sasa wameula, hasa kama watakuwa kweli wanataka mambo yabadilike baada ya bilionea wa Ivory Coast aliyesaidia kukua kwa kipaji cha Gervais Lombe Yao, maarufu kama Gervinho, kusema yupo tayari kuwapa kipa au wachezaji wengine nyota.

Gervais Lombe Yao 'Gervinho'.
Pamoja na Yanga, bilionea huyo, Aziz Alibhai, mwenye asili ya Tanzania, amesema pia yupo tayari kuwatoa wachezaji wake kwa mkopo au kwa makubaliano tofauti ili kusaidia timu za Tanzania.

“Nina kipa anaitwa Badra Ali (Sangare),…

Na Saleh Ally
YANGA sasa wameula, hasa kama watakuwa kweli wanataka mambo yabadilike baada ya bilionea wa Ivory Coast aliyesaidia kukua kwa kipaji cha Gervais Lombe Yao, maarufu kama Gervinho, kusema yupo tayari kuwapa kipa au wachezaji wengine nyota.

Gervais Lombe Yao 'Gervinho'.
Pamoja na Yanga, bilionea huyo, Aziz Alibhai, mwenye asili ya Tanzania, amesema pia yupo tayari kuwatoa wachezaji wake kwa mkopo au kwa makubaliano tofauti ili kusaidia timu za Tanzania.
“Nina kipa anaitwa Badra Ali (Sangare), huyu ni kipa wa pili wa timu ya taifa. Angalia anacheza timu ya daraja la kwanza lakini sasa yuko timu ya taifa.  Ni kati ya makipa watatu tuliokuja nao hapa.
“Nimepewa taarifa Yanga wanahitaji kipa, wanaweza kuja tukazungumza ili nijue wanamhitaji kwa mkopo au tofauti. Lengo langu apate uzoefu zaidi kwa kuwa bado ana nafasi ya kucheza Ulaya,” alisema Alibhai, aliyezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 1950 jijini Dar es Salaam.
Alibhai ambaye ni mmiliki wa Shule ya Kukuza Vipaji ya Ivoire Academie ambayo ilimkuza mshambuliaji Gervinho wa Arsenal, alisisitiza anataka kufanya hivyo kwa ajili ya uzalendo wake na Tanzania pamoja na wachezaji wake.
“Najua suala hili litakuwa na msaada kila upande wa Tanzania kwa kuwa bado ni taifa langu, nilizaliwa hapa. Lakini wachezaji wangu pia kwa kuwa nataka wapate mafanikio kama ilivyokuwa kwa Gervinho au wengine wengi wanaocheza Ulaya sasa,” alisema Alibhai.
“Nimesikia kuna wachezaji wa Ivory Coast wanacheza hapa (Kipre na Bolou Tchetche). Hivyo naweza pia kusaidia kuendeleza soka ya Tanzania na mambo yakaenda vizuri.”
Bilionea huyo aliyewahi kumiliki timu nchini Ubelgiji, alisema kazi ya kuendelea na majadiliano hayo ameiacha kwa wakala wa kuuza wachezaji wa hapa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
“Wakati mwingine mimi ni mtu ambaye niko ‘busy’ sana kwa kuwa nafanya biashara nyingi. Hivyo wakala huyo atawasiliana na Yanga na Simba wakiwa tayari wanaweza kuja Abidjan wakawaona vijana na pia wakasema wanamhitaji yupi, halafu tufanye makubaliano,” alisema.
Alibhai alikuwa kati ya watu waliokuwa katika msafara wa timu ya Ivory Coast iliyokuja nchini kupambana na Taifa Stars katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia nchini Brazil, mwakani.

No comments:

Post a Comment