Tuesday, June 18, 2013

KUELEKEA PAMBANO LA SIMBA VS YANGA…WABUNGE WALA MSOTO JAMHURI

Posted by GLOBAL on June 18, 2013 at 1:41pm 0 Comments
WABUNGE kutoka majimbo mbalimbali nchini, mwishoni mwa wiki iliyopita walidamkia na kwenda Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kujiandaa na mechi yao ya Simba na Yanga, itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika kilele cha Tamasha la Matumaini.

Julai 7, mwaka huu (Sabasaba), litafanyika lile tamasha la kihistoria la Usiku wa Matumaini ambalo hupambwa na matukio mengi ya burudani na michezo, mojawapo likiwa la mechi ya soka ya wabunge ambapo mashabiki wa Simba watamenyana na watani zao Yanga.

Katika kuhakikisha wanakuwa ‘fiti’, wabunge hao, wapo kwenye program ya mazoezi ya kila siku asubuhi, lengo likiwa moja tu kushinda mtanange huo. Simba wanajiweka sawa ili wawafunge Yanga, vilevile upande wa Yanga wanataka kukata vilimilimi vya Simba.

Mechi kama hiyo, ilifanyika Uwanja wa…

Mechi kama hiyo, ilifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Julai 7, mwaka jana, katika kilele cha Tamasha la Usiku wa Matumani 2012.
Mazoezi ya asubuhi yanasimamiwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, anayeshughulikia elimu, Kassim Majaliwa.
Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Majaliwa alisema, amelazimika kuwahenyesha wabunge kwa takriban saa tatu ili wawe vizuri.
“Tunataka pale Uwanja wa Taifa siku ya Sabasaba mashabiki wa Simba na Yanga waone soka safi, ndiyo maana umeona nimewapa mazoezi ya nguvu sana,” alisema Majaliwa na kuongeza:
“Pia, tutacheza mechi mbili za kirafiki pamoja, baada ya hapo, Simba na Yanga watajigawa, kila upande utatengeneza kambi yake.”
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Idd Azzan alisema kuwa soka la Simba na Yanga mwaka huu, litakuwa na ushindani mkubwa.
“Mwaka jana Yanga walifungwa, kwa hiyo mwaka huu wanataka kurekebisha makosa. Upande mwingine, Simba nao wanataka kuonesha kwamba mwaka jana hawakubahatisha,” alisema Azzan.
Akaongeza: “Kila shabiki wa soka nchini, anaelewa kuwa msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Simba, kwa hiyo wabunge wa Simba wanataka kuwafunga Yanga ili kufidia machungu ya Simba kufungwa na Yanga, vilevile kupoteza ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.”

No comments:

Post a Comment