Thursday, March 27, 2014

Vita dhidi ya Polio vimefaulu duniani

 
Katika baadhi ya nchi kama Pakistan, wahudumu hupigwa risasi wanapotoa chanjo dhidi ya Polio
Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa asilimia themanini ya watu wote duniani wako salama kutoka kwa ugonjwa wa kupooza au Polio.
Hii ni kutokana na kutokuwepo visa vipya vya ugonjwa huo nchini India katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
WHO linasema kuwa ugonjwa huo umeangamizwa eno zima la kusini mashariki mwa Asia likiwemo taifa la India.
Tangu miaka ya tisini kampeni kubwa ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio imeendeshwa nchini India ambapo watoto milioni mia moja na sabini wamepata chanjo.
Hali hii inaonekana kuwa ushindi mkubwa kwenye vita dhidi ya ugonjwa huo hatari.
Hata hivyo ugonjwa wa Polio ambao unaweza kusababisha ulemavu unaendelea kuripotiwa nchini Pakistan, Afghanistan na Nigeria.

No comments:

Post a Comment